LimaNami icon

LimaNami

Afrosoft Limited
Free
100+ downloads

About LimaNami

LimaNami ni nini?
LimaNami ni mtandao wa uwekezaji katika mnyororo mzima wa thamani kwenye sekta ya kilimo biashara. LimaNami imejikita zaidi katika utatuzi wa changamoto zinazowakabili wajasiriamali katika uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mazao ya chakula.

Kwanini LimaNami?
Watu wengi wanatamani kulima kibiashara, lakini wengi wao wanakumbana na changamoto za upatikanaji wa ardhi inayofaa kwa ajili ya kilimo, mtaji na ushauri wa kitaalamu. Aidha, wachache wanaojaribu kukabiliana na changamoto hizo na nyinginezo kama hizo bado wanakumbana na changamoto katika huduma za usafirishaji na soko la uhakika kwa ajili ya mazao yao.

LimaNami itakusaidiaje?
LimaNami itakuwezesha kupata huduma za kilimo na mifugo zikiwemo ardhi inayofaa kwa ajili ya kilimo, mtaji na ushauri wa kitaalam. Pia, itakuunganisha na huduma za usafirishaji na masoko ya uhakika kwa ajili ya mazao yako ndani na nje ya Tanzania.

Je, LimaNami ina malengo gani ya muda mrefu?
LinaNami inalenga kupunguza umasikini wa kipato na uhaba wa chakula nchini Tanzania, barani Afrika na duniani kote kwa kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao yote ya chakula nchini na kuinua uchumi wa wakulima wadogo na wa kati hasa waishio vijijini na kukuza mitaji ya wawekezaji katika sekta ya kilimo.

LimaNami Screenshots