Ni Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya vyama vya wafanyakazi no 10 ya mwaka 1998, na kilipewa nambari ya usajili 010 tarehe 15/09/2000. TALGWU inaunganisha wafanyakazi wote waliopo chini ya Mamlaka za serikali za mitaa na Taasisi nyingine nchini ambapo hadi kufikia June 2018, Chama kilikuwa na wanachama 62,170.
TALGWU inajishirikisha na shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ,shirikisho la vyama vya wafanyakazi vinavyotoa huduma kwa umma duniani (PSI) na Mtandao wa Vyama vya Wafanyakazi vya Serikali za Mitaa Africa (AMALGUN). Hivyo basi chama cha wafanyakazi ni ummoja, muungano, na mshikamano wa wafanyakazi ambao nia, malengo, matakwa na matarajio yao yanafanana.
Umoja huo ndio nguzo pekee ya kupatia ufumbuzi wa matatizo yao.
TALGWU inaelimisha, inatetea, na kulinda ajira na ujira wa wanachama wake kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na nyaraka mbalimbali za kazi.

Show More