sokonisasa icon

sokonisasa

Marlekano
Free
100+ downloads

About sokonisasa

App hii inawaunganisha WAZALISHAJI wa mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, WANUNUZI wa mazao hayo, WASAFIRISHAJI wa mazao hayo, MADUKA YA PEMBEJEO, TAASISI ZA FEDHA na za Kiraia (NGO), VYUO vya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na WATAALAMU wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika mikoa yote TANZANIA.

App hii inawezasha MAKUNDI haya WAZALISHAJI, WANUNUZI, WASAFIRISHAJI, MADUKA YA PEMBEJEO, WATAALUM, TAASISI za FEDHA, NGO kusajili taarifa zoa na namna wanavyoweza kupatikana ili kuwasiliana kwa urahisi popote walipo Tanzania kuanzia ngazi ya KATA, WILAYA na MKOA na kuwawezesha kufanya BIASHARA kwa urahisi zaidi wakati wowote.

WAZALISHAJI kuonyesha mazao yao, bei, mahali walipo, kiasi walichonacho na wanavyoweza kupatikana.

WANUNUZI wanaweza kununua au kuonyesha wapi walipo, kiasi wanachohitaji na bei wanayoweza kununua mazao.

MADUKA YA PEMBEMBEJEO kuonyesha mahali gani walipo aina na bei ya pembejeo walizonazo.

WATAALAMU wa kilimo, uvuvi na mifugo kuonyesha huduma ya utaalamu wanaotoa na mahali wanapopatikana.

WASAFIRISHAJI kuonyesha mahali walipo, gharama wanazotoza na uwezo wa chombo cha usafirishaji.

TAASISI YA FEDHA NA NGO kuonyesha aina za huduma wanazotoa na namna wanavyopatikana

VYUO vya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuonyesha huduma, utaalamu na mafunzo wanayotoa na mahali wanapopatikana.

Kupitia App hii utapata DONDOO za KILIMO, MIFUGO, UVUVI na BIASHARA

sokonisasa Screenshots

More from Marlekano