Shule Direct Kids icon

Shule Direct Kids

Shule Direct
Free

About Shule Direct Kids

Shule Direct Kids ni app iliyobuniwa kwa ajili ya matumizi ya watoto wa shule za msingi nchini Tanzania. App inamsaidia mtoto wa darasa la kwanza hadi la saba, kujifunza na kuongeza umahiri wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa kutumia michezo iliyotengenezwa kutokana na mtaala na muongozo wa elimu ya msingi nchini Tanzania.

Mzazi tumia App hii kupata taarifa ya maendeleo ya mtoto wako pia kumsaidia kuyamudu zaidi masomo yake au yale maeneo yanayompa changamoto. App hii pia inakusaidia mzazi kufahamu mambo yote anayotakiwa kujifunza mtoto wako pindi awapo shuleni.

FAIDA ZA SHULE DIRECT KIDS
- Kupenda kujifunza
- Kujifunza kwa Uhuru, Muda Wowote, Mahali Popote
- Nyenzo zinazofuata mtaala wa Taifa wa Elimu ya Msingi darasa la 1 - 7
- Kujifunza matumizi sahihi na salama ya teknolojia na mifumo yake
- Kumfanya mtoto kuwa mbunifu zaidi
- Kuweka kumbukumbu na taarifa zote za mtoto, kumsaidia mzazi kupata ripoti kwa haraka na kufuatilia kwa karibu
- Kuongeza ufaulu


Pakua Shule Direct Kids App sasa BURE!


KUHUSU SHULE DIRECT
Shule Direct ni shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania lililojikita kwenye matumizi ya teknolojia na mifumo yake katika kuongeza wigo na fursa za upatikanaji wa nyenzo bora za kujifunzia kwa wanafunzi na walimu wa shule za msingi na sekondari ili kuongeza ufaulu na matokeo chanya ya elimu. Tunafanya kazi na walimu bora wanaokidhi vigezo vya ufundishaji, kutengeneza nyenzo za kujifunzia katika mifumo ya notes, chemsha bongo, mafumbo na michezo mbalimbali kwa kufuata mitaala na miongozo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa elimu ya msingi na sekondari. Nyenzo zetu zinapatikana kwa njia mbalimbali zikiwemo application za simu, mtandao wa www.shuledirect.co.tz mfumo wa offline Learning Management System (LMS) pamoja na njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS).

WASILIANA NASI
Kama una swali, maoni, ushauri, au unahitaji msaada au taaria zaidi, wasiliana nasi kupitia info@shuledirect.org Tushirikiane kwa mafanikio ya mtoto wa Tanzania.

Shule Direct Kids Screenshots

More from Shule Direct